Posts

Showing posts from June 7, 2017

Vodacom kuvunja rekodi ya mauzo ya DSE soko la awali

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao WAWEKEZAJI zaidi ya 40,000 wamevutiwa na hisa za Vodacom Tanzania PLC zinazoendelea na mchakato wa kuingia sokoni. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, alisema hisa hizo zitakuwa za kihistoria na zitavunja rekodi kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa miaka 19 tangu kuanzishwa kwake. Hii imechangia kwa kiasi kikubwa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka kuona Watanzania wanakuwa wamiliki wa kampuni kubwa zinazofanya biashara nchini. Biashara katika hisa za Vodacom Tanzania PLC kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam inatarajiwa kuanza mwezi huu baada ya kukamilika kwa taratibu za uhakiki unazofanywa na Mamlaka ya Masoko na Mitaji Tanzania (CMSA). Katika taarifa yake, Ferrao alisema, “Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni ya mawasiliano inayoongoza hapa Tanzania na ndiyo maana leo hii tumekuwa kampuni ya kwanza kutimiza masharti...

Hans Poppe: Simba kaeni mkao wa kula usajili

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe amesema usajili wao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom unakwenda vizuri na wanatarajia kupata wachezaji wote waliopanga kuwa nao. Simba imepanga kusajili wachezaji sita wapya kuimarisha kikosi chake kitakachoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) na Ligi Kuu Vodacom. Hans Poppe alisema jana, mazungumzo na nyota hao yanakwenda vizuri na kilichobaki ni kukamilisha makubaliano ya mishahara huku wakisubiri dirisha la usajili kufunguliwa ili wawasilishe majina Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). “Unajua dirisha la usajili halijafunguliwa. Kinachofanyika hivi sasa ni mazungumzo ya makubaliano na ikiwezekana kusaini mkataba wa awali ili wakati dirisha likifunguliwa, iwe kazi rahisi kukamilisha taratibu nyingine,” alisema. Hata hivyo, Poppe alikat...

Azam yaipiga bao Yanga usajili

Image
Jafari Idd UJANJA ni kupata sio kuwahi! Hivyo ndivyo usemi wa Kiswahili ulivyodhihirika baada ya jana Azam kumsajili mchezaji wa Toto Africans ya Mwanza aliyekuwa asajiliwe na Yanga. Yanga awali walifanya mazungumzo na mchezaji wa Toto Africans, Wazir Junior lakini ameishia kusajiliwa na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili. Licha ya timu yake kushuka daraja, Junior alikuwa ni mwiba kwa baadhi ya timu zilizoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita baada ya kuifungia timu yake mabao saba na kusaidia mabao sita. Akizungumza baada ya kutambulishwa na uongozi wa Azam FC jana, Junior ambaye amekabidhiwa jezi namba saba alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga na klabu nyingine lakini ameamua kujiunga na Azam kukuza kupaji chake. “Nilifanya mazungumzo na Yanga lakini nimeamua kujiunga na Azam. Nimefurahi kujiunga nayo na naamini itanisaidia kutoka hatua moja hadi nyingine,”alisema. Junior (22) alisema anahitaji ushirikiano wa ma...

Wachezaji wa kigeni Yanga, Simba wazua zogo bungeni

Image
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma. WACHEZAJI wa kigeni wanaochezea timu za Yanga na Simba na nyingine kadhaa za Ligi Kuu ya soka ya Vodacom wamezua jambo bungeni mjini Dodoma baada ya wabunge kudai wanaua soka la Tanzania. Hata hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe aliliambia Bunge kuwa madai hayo si ya kweli kwani wachezaji wa kigeni walioshiriki ligi hiyo ni 35 tu. Baadhi ya wachezaji wa kigeni walioko Yanga ni Thaban Kamusoko (Zimbabwe), Obrien Chirwa (Malawi), Haruna Niyonzima (Rwanda), Vincent Bossou (Togo). Wachezaji wa kigeni walio Simba ni Besela Bukungu (Congo DRC), James Kotey(Ghana), Juuko Murshi (Uganda), Laudit Mavugo (Burundi), James Abiey (Ghana). Wachezaji hao walisababisha wabunge kuhoji kama uwepo wao una athari kwa kiwango cha soka la wachezaji wazawa. Waziri Mwakyembe alilieleza Bunge kuwa kati ya wachezaji 112 ambazo timu za Ligi Kuu ya Vodacom ziliruhusiw...

Simba yaikwepa Yanga SportPesa Super Cup

Image
Beki wa Simba, Feston Munezero (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Nakuru All Stars, Mukhwana Sadiky katika mchezo wa SportPesa Super Cup uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Simba ilifungwa kwa penalti 5-4. (Picha na Rahel Pallangyo). WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, Simba, wameyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kufungwa na timu isiyo na jina ya Nakuru All Stars ya Kenya kwa penalti 5-4. Matokeo hayo ya kufungwa kwa Simba sasa yanaifanya timu hiyo kuwakwepa watani zao wa jadi, Yanga, ambayo juzi walitinga nusu fainali. Yanga jana walikaririwa wakisema kuwa wanataka kukutana na Simba katika fainali ya mashindano hayo ili kuishikisha adabu timu hiyo iliyomaliza ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, timu hizo zilitoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na kumsaka mshindi kwa matu...

RC Mghwira: Mimi sio mpinzani wa maendeleo

Image
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira huku Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wakuu wa wilaya za Kinondoni, Ubungo na Ilala wakipiga makofi. (Picha na Ikulu). MKUU mpya wa Mkoa wa Kilimanajaro, Anna Mghwira, amemhakikisha Rais John Magufuli na Watanzania kwa jumla kuwa katu yeye sio mpinzani katika masuala yanayohusu maendeleo na maslahi ya taifa. Aliyasema hayo jana Ikulu katika hafla ya kuapa mbele ya Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya Rais kumteua hivi karibuni kuziba nafasi ya Said Meck Sadick aliyemwomba Rais kujiuzulu akisisitiza kuwa, changamoto za kiafya alizo nazo hazitamwezesha kuendana na kasi ya maendeleo katika Serikali ya Awamu ya Tano. Mghwira alisema anavyofahamu yeye ni kwamba, kazi za mkuu wa mkoa...

Mauaji mengine Kibiti askari mgambo apigwa risasi 3 akiwa uvunguni na kufariki dunia.

Image
Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani hapa,  Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku akiwa nyumbani kwake.Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon amesema watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00  usiku kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.Simon amesema baada ya watu hao  kuingia ndani walipitiliza moja kwa moja hadi kwenye chumba chake ambapo walimkuta mkewe marehemu na kumhoji alipo mumewe. Amesema baada ya kuona mkewe hataji mahali alipo mumewe walianza kumtafuta ndani ya nyumba yake na kufanikiwa kumuona marehemu akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda ndipo wakamfyetulia risasi na kuondoka.Simon amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote. Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Dk Iddy ...