Posts

Showing posts from June 14, 2017

Cabo Snoop-AWAA

Image

Gari lenye kasi zaidi duniani latarajiwa kufanyiwa majaribio Oktoba

Image
  Gari lenye mwendo wa kasi zaidi duniani litakimbia kwa mara ya kwanza kabisa tarehe 26 mwezi Oktoba,Gari litakimbia kwa kasi ya chini wakati wa majiribio kwenye uwanja wa ndege wa Newquay huko Conawall. Wahandisi wanataka kukagua mitambo yote ya gari hilo kabla ya kulipeleka nchini Afrika Kusini mwaka ujao, kukimbia kuvunja rekodi ya mbio ya kasi zaidi ardhini. Kwa sasa rekodi ya kasi ardhini ni 763mph au 1,228km/h, na gari hilo linalofahamika kama Bloodhound litaongeza kasi kwanza hadi 800mph na kisha 1000mph.Majaribio ya Newquay hayatafikia kasi kama hiyo kwa kuwa barabara ya mita 2,744 ni fupi kiliwezesha Bloodhound kushika kasi. Badala yake dereva Andy Greren, ataliendesha gari hilo kwa kasi ya 200mph likitumia injini ya ndege aina ya Eurofighter-Typhoon.Itakua siku ngumu kwa Dereva Andy Green kwa sababu itakuwa mara yake ya kwanza kuliendesha gari hilo. Matarajio ni kuwa Bloodhound litapelekwa eneo la Hakskeen Pan huko Northen C...

JPM asema Barrick ni wanaume,wametubu na wamekubali kulipa kila kitu.

Image
Prof.John Thornton ( MMILIKI WA ACACIA MINING LIMITED )akiwa na Dr. John Pombe Magufuli Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jijini Dar es salaam leo hii. Rais John Pombe Magufuli (JPM) amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni mama ya uchimbaji wa madini ya Barrick Canada, Profesa John Thornton na kufanya naye mazungumzo Ikulu leo. Amesema Barrick imepitia mapendekezo yote ya kamati ya pili ya mchanga wa madini na kuwa imekubali kulipa chochote ambacho kitaonekana wanatakiwa kulipa.“Baada ya kuwaona nilifurahi na nikasema hawa ni wanaume, wakasema yaliyotokea ni bahati mbaya na wanatubu kwa hayo.” Amesema. Rais amesema Mkurugenzi huyo alikuja na timu yake ya wanasheria wakati kwa upande wa Tanzania nao ilikuwepo timu ya wanasheria wakiongozwa na Profesa  Palamagamba Kabudi.“Ilikuwa ni timu ya maprofesa kwa maprofesa,” amesema.Amesema timu hiyo ya Barrick ilipitia mapendekezo yote na wakakubali kuwa wapo tayari kulipa baada ya majadiliano na makub...