Jukwaa la Biashara kuiandaa Tanga na fursa za bomba
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Dk Jim Yonazi. WIKI ya kuelekea k w e n y e Jukwaa la biashara mkoani Tanga inaanza kesho huku Mkuu wa Mkoa wa huo, Martine Shigela akisema jukwaa hilo litasaidia kuwaandaa wakazi wa mkoa wake kushiriki kikamili kwenye fursa zinazokuja na bomba la mafuta. Agosti 5, mwaka huu, Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni waliweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga linalotarajiwa kuibua fursa nyingi za uwekezaji, mbali na ajira.Akizungumza katika mahojiano maalumu na timu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Shigela alisema Jukwaa hilo litakalorindima Alhamisi ijayo, Agost 17 mwaka huu, mbali na kuwaandaa wana Tanga kifikra, litatumika pia kutangaza fursa zinazopatikana mkoani humu. Hili ni jukwaa la tatu kuandaliwa na TSN inayochapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo. La kwanza lilifanyika Mkoani Simiyu mwezi Februri na la...