Posts

Showing posts from March 9, 2018

Diamond atangaza kufunga ndoa mwaka huu

Image
Diamond na mama yake Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ametumia siku ya jana ya Wanawake Duniani kumtakia kheri mama yake mzazi na kutangaza mipango yake ya ndoa. Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu ametumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram kufikisha ujumbe huo kwa mama yake huku akiweka wazi mpiango yake ya kuvuta jiko mwaka huu. Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini…..Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya...

MAGAZETI YA LEO TAR:09/3/2018

Image
Kama una tangazo lolote   TUWASILIANE KWA NAMBA: +255 757634776 ,+255 625953090

Trump akubali mualiko wa kukutana na Rais wa korea kusini Kim Jong Un.

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini. Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale. Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini. Kim pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake makombora,msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao rais huyo Kim Jong Un. Hatua hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongoz...