Ripoti tanzanite, almasi sasa kutikisa mawaziri
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Taarifa ya Kamati Maalumu ya Bunge ya kuchunguza madini ya tanzanite na almasi kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye hafla iliyofanyika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Anayeshuhudia ni Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. (Picha na Mroki Mroki). UKO uwezekano mkubwa wa Baraza la Mawaziri kutikisika baada ya mawaziri kadhaa waliopo na wale walioondolewa kutajwa mara kadhaa katika taarifa za kamati maalumu za bunge kuchunguza biashara ya Tanzanite na almasi. Aidha taarifa zote mbili ziliwataja kwa majina watu kadhaa wakiwemo mawaziri waliopo katika baraza la sasa kwa kujihusisha moja kwa moja katika maamuzi yaliyopindisha sheria na kukiuka utaratibu. Kamati zote mbili zilizungumzia kwa undani hasara kubwa zilizopatikana kutokana na ushauri mbovu na usimamizi dhaifu katika mkataba wa kuuza hisa katika kampuni ya almasi mwaka 1994 ambao hazikusaidiwa na pia ubia wa Stamico na Tanzanite One Mining Limited (TML) a...