Posts

Showing posts from August 14, 2017

Majaliwa: Serikali kulipa madeni yote ya watumishi

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali italipa madeni yote ya watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali. “Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli alisitisha malipo sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika, yale yaliyobainika kuwa ni halali yatalipwa. Tunataka watumishi mfanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa bidii,” alieleza. Alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliofanyika Kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora. Akiwa katika wilaya za Sikonge, Urambo, Kaliua na Uyui, Waziri Mkuu alielezwa na baadhi ya wabunge wa mkoa huo kwamba kuna watumishi ambao walihamishwa kutoka manispaa kwenda wilaya za jirani, lakini hawajalipwa fedha zao kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Kwa nyakati tofauti, Waziri Mkuu ambaye ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wa umma kila anapofanya ziara za...