Posts

Showing posts from August 21, 2017

Je wazijua Bahari Mbili Zinazokutana Lakini Maji 'Hayachanganyikani'?

Image
U MEONA picha na video zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mahali ambapo bahari mbili zinakutana lakini bado maji yake yanaonekana kutochanganyika?  Kama hujaona basi kwa taarifa yako, bahari mbili za Atlantic na Pacific, kuna sehemu zinakutana lakini cha ajabu, maji yanaonekana ‘kutochanganyika’, upo mpaka kabisa katika maji, unaoyatofautisha maji ya bahari moja na bahari nyingine, ya upande mmoja yakionesha kuwa na rangi tofauti na ya upande wa pili. Wengine wanalihusisha tukio hili na nguvu zisizoonekana, wengine wanaeleza ni miongoni mwa ishara kwamba Mungu yupo na wengine hawaelewi chochote. Lakini nini hasa kinachosababisha hali hii? Kuweka mambo sawa, lazima ieleweke kwamba si kwamba maji ya bahari hizo mbili hayachanganyikani, isipokuwa huchukua muda fulani kuchanganyikana. Kwa sababu gani? Pacific ndiyo bahari kubwa kuliko zote duniani, ikikusanya maji kutoka Antarctica mpaka Arctic, kuanzia ncha ya Kaskazini mpaka...

Asali Yenye Miaka zaidi ya 2000 Yakutwa Kwenye Mapiramidi ikiwa na virutubisho vyote.

Image
M APIRAMIDI ya Misri ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia lakini ndani yake, kumegunduliwa maajabu mengine yaliyowashangaza wengi.  Mwaka 2006, wataalamu wa mambo ya kale waliokuwa wakifanya utafiti kwenye mapiramidi hayo, waligundua kitu kilichowashangaza sana. Ndani ya moja ya mapiramidi hayo, walikuta chungu kikubwa, kikiwa na asali. Uchunguzi wao ulionesha kwamba asali na chungu hicho, vimekaa eneo vilipokutwa kwa zaidi ya miaka 2000 lakini cha ajabu, asali bado ilikuwa nzima na waliopata fursa ya kuionja, walikiri kwamba ilikuwa na ladha halisi ya asali na usingeweza kuitofautisha na asali iliyotoka kurinwa muda huo. Jambo hilo liliwashangaza sana wote waliokuwa kwenye utafiti huo ambapo ili kujiridhisha, ilibidi chungu hicho kitolewe na kupelekwa maabara ambapo uchunguzi wa kina ulianza kufanyika. Kilichobainika, ni kwamba licha ya asali hiyo kukaa miaka yote hiyo, bado haikupoteza sifa yake hata moja, ilikuwa katika ubora wake na ingeweza kutu...

Fahamu kuku wa maajabu aina ya 'Ayam Cemani' wenye nyama na mifupa myeusi

Image
Unaweza ukashangaa ila ndiyo hivyo kuwa Mungu ameumba viumbe wengi ambao pengine katika maisha yako viumbe wengine hutaweza kuwaona lakini sio kwa kuku aina ya Ayam Cemani ambao kila kitu kutoka kwenye miili yao ni cheusi kuanzia manyoya yao, Nyama na hadi mayai wanayototoa wakati mwingine.Kuku hao ambao wanapatikana kwa wingi nchini Indonessia walianza kugundulika karne ya 17 kwenye visiwa vya Java na walikuwa wakitumika zaidi kwenye imani za kidini kwa kuwaabudu kuku hao. Kuku hao ambao hata viungo vya ndani kama ulimi,utumbo na mifupa vyote vina rangi nyeusi walianza kuingia kwa mara ya kwanza barani Ulaya mnamo mwaka 1998 kwa ajili ya utafiti wa kibiolojia kwenye za Uholanzi, Ujerumani, Slovakia na Czech Republic. Asili ya jina la kuku hao linatokana na kijiji ambacho kuku hao walianza kupatikana karne 12 yaani Ayam maana yake ‘Chickens’ na Cameni ni kijiji kilichopo kwenye kisiwa cha Java huko Indonessia. Kwa mujibu wa mfugaji na mtalaamu wa...