Asali Yenye Miaka zaidi ya 2000 Yakutwa Kwenye Mapiramidi ikiwa na virutubisho vyote.
MAPIRAMIDI ya Misri ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia lakini ndani yake, kumegunduliwa maajabu mengine yaliyowashangaza wengi.
Mwaka
2006, wataalamu wa mambo ya kale waliokuwa wakifanya utafiti kwenye
mapiramidi hayo, waligundua kitu kilichowashangaza sana. Ndani ya moja
ya mapiramidi hayo, walikuta chungu kikubwa, kikiwa na asali.
Uchunguzi
wao ulionesha kwamba asali na chungu hicho, vimekaa eneo vilipokutwa
kwa zaidi ya miaka 2000 lakini cha ajabu, asali bado ilikuwa nzima na
waliopata fursa ya kuionja, walikiri kwamba ilikuwa na ladha halisi ya
asali na usingeweza kuitofautisha na asali iliyotoka kurinwa muda huo.
Jambo
hilo liliwashangaza sana wote waliokuwa kwenye utafiti huo ambapo ili
kujiridhisha, ilibidi chungu hicho kitolewe na kupelekwa maabara ambapo
uchunguzi wa kina ulianza kufanyika.
Kilichobainika,
ni kwamba licha ya asali hiyo kukaa miaka yote hiyo, bado haikupoteza
sifa yake hata moja, ilikuwa katika ubora wake na ingeweza kutumika kwa
shughuli yoyote kama yalivyo matumizi ya kawaida ya asali.
Hata
hivyo, uchunguzi zaidi kwenye chungu hicho, ulibaini mabaki ya mifupa
ya mtoto mdogo, yaliyokuwa chini kabisa ya chungu, ambayo hayakuwa
yamecha-nganyikana na asali hiyo.
Baadaye,
ikaja kubainika kwamba watu walioishi kwa kipindi hicho, walikuwa na
utamaduni wa kuwatoa kafara watoto wachanga, hasa wa kiume kwa kuwaua
kisha kuiweka miili yao kwenye vyungu vikubwa vilivyojaa asali, kama
sadaka kwa miungu yao ili kuwakinga na mabalaa mbalimbali.
Ili
kujiridhisha zaidi, watafiti hao walirudi tena kwenye mapiramidi ambapo
walifanikiwa kupata vyungu vingine kadhaa, vikiwa na asali ambayo chini
ilikuwa na mabaki ya mifupa ya watoto, lakini yenyewe ikiwa kwenye
ubora wake uleule.
Kitaalamu,
inaelezwa kwamba asali ndiyo chakula pekee kisichoweza kuharibika. Hii
ni kwa sababu, asali ina mchanganyiko wa kipekee wa maji na virutubisho
vingine, ambavyo kwa pamoja hufanya kiwango cha asidi (pH) kuwa kati ya
3.2 hadi 4.5.
Comments