Manji anaumwa, ashindwa kufika kortini
Katikati ni Yusuf manji ambae kwa sasa ni mgonjwa IMELETWA KWENU NA DITRO JOSIA @ www.wakisasa.blogspot.com MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kusikiliza utetezi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabishara Yusuf Manji baada ya kuelezwa kuwa anaumwa. Wakili wa mshitakiwa, Hajra Mungula alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa kesi imekuja kwa ajili ya utetezi lakini wamepata taarifa kuwa mshitakiwa hajafika. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya utetezi. Mahakama hiyo ilitakiwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo jana kwa upande wa utetezi ambapo tayari shahidi mmoja ameshatoa ushahidi wake. Wakati huo huo, katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Manji na wenzake watatu, imeahirishwa hadi Septemba 8, mwaka huu kwa sababu hiyo hiyo. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias ...