Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru IMELETWA KWENU NA DITRO JOSIA @ www.wakisasa.blogspot.com BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa siku saba kuanzia Septemba 4, 2017 hadi 11, mwaka huu ili waombaji wenye sifa wawasilishe maombi yao kabla ya kufungwa kwa dirisha la maombi. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mchakato wa uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/18 na kwamba HESLB imetenga jumla ya Sh bilioni 427 kwa mikopo yote. Kwa mujibu wa Badru, jumla ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2017/18, wanatarajiwa kupata mikopo ya elimu ya juu huku wanafunzi 93,292 wakiwa wanaendelea kupokea mikopo hiyo kwa ajili ya kukamilisha masomo yao. Badru alisema hadi kufikia juzi, jumla ya waombaji wa mikopo kwa njia ya mtandao walikuwa 49,282, kati yao waombaji 15,473 wakiwa wamekamilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kwa kufuata taratibu zo...