Fahamu kuku wa maajabu aina ya 'Ayam Cemani' wenye nyama na mifupa myeusi
Unaweza
ukashangaa ila ndiyo hivyo kuwa Mungu ameumba viumbe wengi ambao
pengine katika maisha yako viumbe wengine hutaweza kuwaona lakini sio
kwa kuku aina ya Ayam Cemani ambao kila kitu kutoka kwenye miili yao ni
cheusi kuanzia manyoya yao, Nyama na hadi mayai wanayototoa wakati
mwingine.Kuku hao ambao wanapatikana kwa wingi nchini Indonessia
walianza kugundulika karne ya 17 kwenye visiwa vya Java na walikuwa
wakitumika zaidi kwenye imani za kidini kwa kuwaabudu kuku hao.
Kuku
hao ambao hata viungo vya ndani kama ulimi,utumbo na mifupa vyote vina
rangi nyeusi walianza kuingia kwa mara ya kwanza barani Ulaya mnamo
mwaka 1998 kwa ajili ya utafiti wa kibiolojia kwenye za Uholanzi,
Ujerumani, Slovakia na Czech Republic.
Asili
ya jina la kuku hao linatokana na kijiji ambacho kuku hao walianza
kupatikana karne 12 yaani Ayam maana yake ‘Chickens’ na Cameni ni kijiji
kilichopo kwenye kisiwa cha Java huko Indonessia.
Kwa
mujibu wa mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ndege wanaoliwa Bw. Paul
Bradshaw kutoka Marekani kwenye mahojiano yake na mtandao wa Greenfire Farm amesema mayai yake yana virutubisho mara mbili ya kuku wa kawaida na pia hata nyama yake ina utofauti kidogo na kuku wa kawaida.
Hata
hivyo mtaalamu huyo amesema wateja wengi wanaulizia nyama yake wengi
wao wakiamini kuwa ulaji wa nyama hiyo huongeza kinga ya mwili.
Ingawaje
bado hakuna tafiti zozote za kibailojia kuhusu ukweli huo mpaka sasa
lakini watu wengi wa Indonesia wanaamini ulaji wa mayai mabichi ya kuku
hao huondoa sumu mwilini na ni tiba kwa akina mama wanaoshikwa na
uchungu wa uzazi kwa muda mrefu.
Mpaka
sasa ni utafiti mmoja tuu uliofanywa na Mwanasayansi, Jan Steverink
kutoka Uholanzi ambaye alibaini kuwa rangi nyeusi ya kuku hao inatokana
na ongezeko la rangi kwenye tishu baada ya mabadiliko ya kijenetiki
yajulikanayo kwa lugha ya kitaalamu kama (Fibromelanosis).
Kuku
hao ambao wamejizolea umaarufu nchini Indonesia wamempa jina la gari la
kifahari aina Lamborghini na hao wanamuita ‘Lamborghini of poultry’.
Kwa
bei ya Marekani yai moja la kuku hao huuzwa mpaka dola 130 sawa na Tsh
laki 2.9k, huku kuku mzima akiuzwa dola 2,500 sawa na Shilingi milioni
5.5 za kitanzania.
Comments