Gari lenye kasi zaidi duniani latarajiwa kufanyiwa majaribio Oktoba
Gari
lenye mwendo wa kasi zaidi duniani litakimbia kwa mara ya kwanza kabisa
tarehe 26 mwezi Oktoba,Gari litakimbia kwa kasi ya chini wakati wa
majiribio kwenye uwanja wa ndege wa Newquay huko Conawall.
Wahandisi
wanataka kukagua mitambo yote ya gari hilo kabla ya kulipeleka nchini
Afrika Kusini mwaka ujao, kukimbia kuvunja rekodi ya mbio ya kasi zaidi
ardhini.
Kwa sasa rekodi ya kasi ardhini ni 763mph au 1,228km/h, na gari hilo linalofahamika
kama Bloodhound litaongeza kasi kwanza hadi 800mph na kisha
1000mph.Majaribio ya Newquay hayatafikia kasi kama hiyo kwa kuwa
barabara ya mita 2,744 ni fupi kiliwezesha Bloodhound kushika kasi.
Badala
yake dereva Andy Greren, ataliendesha gari hilo kwa kasi ya 200mph
likitumia injini ya ndege aina ya Eurofighter-Typhoon.Itakua siku ngumu
kwa Dereva Andy Green kwa sababu itakuwa mara yake ya kwanza kuliendesha
gari hilo.
Matarajio
ni kuwa Bloodhound litapelekwa eneo la Hakskeen Pan huko Northen Cape
nchini Afrika Kusini kwa muda wa mwaka mmoja hivi unaokuja kajaribu
kutimiza lengo lake,Ili hilo liweze kufanyika, awamu nyingine ya uundaji
wa roketi hiyo ni lazima ukamilike.
Eneo lililotengezwa huko Hakskeen kuwezesha Bloodhound kufikia kasi yake
Comments