JPM asema Barrick ni wanaume,wametubu na wamekubali kulipa kila kitu.
Prof.John Thornton(MMILIKI WA ACACIA MINING LIMITED)akiwa na Dr. John Pombe Magufuli Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jijini Dar es salaam leo hii. |
Rais
John Pombe Magufuli (JPM) amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni
mama ya uchimbaji wa madini ya Barrick Canada, Profesa John Thornton na
kufanya naye mazungumzo Ikulu leo.
Amesema
Barrick imepitia mapendekezo yote ya kamati ya pili ya mchanga wa
madini na kuwa imekubali kulipa chochote ambacho kitaonekana wanatakiwa
kulipa.“Baada ya kuwaona nilifurahi na nikasema hawa ni wanaume,
wakasema yaliyotokea ni bahati mbaya na wanatubu kwa hayo.” Amesema.
Rais
amesema Mkurugenzi huyo alikuja na timu yake ya wanasheria wakati kwa
upande wa Tanzania nao ilikuwepo timu ya wanasheria wakiongozwa na
Profesa Palamagamba Kabudi.“Ilikuwa ni timu ya maprofesa kwa
maprofesa,” amesema.Amesema timu hiyo ya Barrick ilipitia mapendekezo
yote na wakakubali kuwa wapo tayari kulipa baada ya majadiliano na
makubaliano yatakayoafikiwa.
Comments