Azam yaipiga bao Yanga usajili

Jafari Idd
UJANJA ni kupata sio kuwahi! Hivyo ndivyo usemi wa Kiswahili ulivyodhihirika baada ya jana Azam kumsajili mchezaji wa Toto Africans ya Mwanza aliyekuwa asajiliwe na Yanga. Yanga awali walifanya mazungumzo na mchezaji wa Toto Africans, Wazir Junior lakini ameishia kusajiliwa na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Licha ya timu yake kushuka daraja, Junior alikuwa ni mwiba kwa baadhi ya timu zilizoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita baada ya kuifungia timu yake mabao saba na kusaidia mabao sita.

Akizungumza baada ya kutambulishwa na uongozi wa Azam FC jana, Junior ambaye amekabidhiwa jezi namba saba alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga na klabu nyingine lakini ameamua kujiunga na Azam kukuza kupaji chake.

“Nilifanya mazungumzo na Yanga lakini nimeamua kujiunga na Azam. Nimefurahi kujiunga nayo na naamini itanisaidia kutoka hatua moja hadi nyingine,”alisema. Junior (22) alisema anahitaji ushirikiano wa mashabiki wa Azam na wachezaji wake na kuwahakikishia hatawaangusha msimu ujao wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd alisema kusajiliwa kwa mchezaji huyo kunatokana na mapendekezo ya Kocha wao, Aristica Cioaba baada ya kuridhika na kiwango chake katika ligi. Alisema Junior ni mchezaji mwenye uwezo lakini amesajiliwa Azam kwenda kugombea namba, hivyo ni lazima apambane kupata nafasi kwenye kikosi chao cha kwanza.

Tayari Azam imesajili wachezaji sita vijana ikiwapandisha kutoka kikosi cha vijana. Wachezaji hao ni Yahaya Zaidi, Stanslaus Rwakatare, Abdallah Haji, Godfrey Elias na Ramadhan Mohamed.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond atangaza kufunga ndoa mwaka huu