Putin: Hakuna atakayepona katika vita vya nyuklia vya Marekani na Russia


Rais Vladimir Putin wa Russia ametahadharisha kuwa, iwapo Marekani itaamua kuingia katika vita vya nyuklia na nchi yake, hakuna upande utakaopona 'kusherehekea' ushindi.Katika mahojiano na Oliver Stone, mtengenezaji filamu wa Marekani, ambapo sehemu ndogo ya mahojiano hayo imepeperushwa na kanali ya televisheni ya Russia Today, Putin amesema: "Sidhani kama kuna yeyote atakayebaki hai kudai kuwa ni mshindi,  katika vita vya silaha za nyuklia kati ya Marekani na Russia."
Kadhalika Rais wa Russia ameutaja Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kuwa chombo cha kuendesha sera za nje za Marekani na nchi yeyote inayojiunga na muungano huo haina budi kuwa mtumwa wa Washington.
Putin amebainisha kuwa, NATO imekuwa ikitafuta 'adui' ili kuhalalisha uwepo wake na ni kwa msingi huo, ndiposa Moscow imekuwa ikijiimarisha kijeshi na kuchua hatua za tahadhari kutokana na chokochoko za muungano huo, ambao umeshadidisha harakati zake katika mipaka ya Russia.

Hivi karibuni, Kamanda wa majeshi ya NATO barani Ulaya, Jenerali Curtis Scaparrotti alikiri kuwa bara hilo sasa limekuwa miongoni mwa maeneo hatari zaidi duniani, ambalo linakabiliwa na changamoto mbili kubwa; za kurejea magaidi kutoka Syria na maeneo mengine, na tishio la ndani la wafuasi wa kundi la kigaidi la Daesh.

Toa maoni yako mdau wangu

Comments

Popular posts from this blog

Diamond atangaza kufunga ndoa mwaka huu