Mgambo mwingine wa pili apigwa risasi kisogoni akivuna ufuta Rufiji'.
Askari
Mgambo, Nurdin Kisinga (33) Mkazi wa Kijiji cha Umwe Kaskazini
Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoani Pwani amelazwa katika Hospital ya
Mchukwi baada ya kupigwa risasi ya kisongoni.Huyu ni mgambo pili kipigwa
risasi ndani ya siku mbili baada ya Erick Mwarabu kuuawa juzi saa tisa
usiku akiwa uvunguni mwa kitanda chake.
Tukio
la jana Jumatano limetokea katika eneo la Ngomboloni lililopo katika
Kijiji cha Umwe Kaskazini ikiwa ni takribani saa 19 tangu Mkuu wa Jeshi
la Polisi(IGP), Simon Sirro kufanya mkutano wa mazungumzo na wazee wa
wilaya za Kibiti na Rufiji ili kukomesha mauaji katika wilaya
hizo.Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, kaka wa majeruhi
aliyejitambulisha kwa jina la Kisinga Athumani Kisinga akiwa katika
Hospitali ya Mchukwi alisema ndugu yake alipigwa risasi akiwa shambani
kwake.
Alisema
Nurdin alikuwa akivuna ufuta wake shambani kwake ndipo watu ambao
hawajajulikana idadi yao walimpiga risasi moja ya kisogoni na kutokomea
kusikojulikana.Kisinga alisema Nurdin alikuwa ameambatana na vijana
wawili ambao ni watoto wake kuvuna ufuta huo.Alisema mara baada ya
kuanguka chini wadogo zake waliomba msaada kwa kupiga yowe na ndipo mtu
mmoja alifika eneo la tukio na kumchukua kwa baiskeli hadi barabarani.
Alisema
mara baada ya kufika barabarani alifanikiwa kubebwa kwa pikipiki hadi
kituo cha Polisi Ikwiriri.Alifafanua kuwa baada ya hapo alikimbizwa
katika kitio cha Afya Ikwiriri ambapo alipatia huduma ya kwanza kituoni
hapo na baadaye alipelekwa Mchukwi kwa matibabu zaidi.Mganga wa zamu
katika hospitali hiyo Emmanuel Humbi alisema wanampeleka kwenye chumba
cha X Ray kwa ajili ya uchunguzi.
Una maoni gani kuhusu hii mdau?
Comments