Majeruhi wa Lucky Vincent atembea kwa mara ya kwanza
Mmoja
wa majeruhi wa ajali ya basi la Shule ya Lucky Vincent, Sadia Ismael
ametembea kwa mara ya kwanza tangu alipopata ajali hiyo Mei 11, mwaka
huu.Ajali hiyo iliyotokea katika eneo Rhotia,Karatu mkoani Arusha,
iligharimu maisha ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja na
kujeruhi wanafunzi watatu ambao walisafirishwa Marekani kwa ajili ya
matibabu.
Wanafunzi
hao ni Sadia, Wilson Tarimo na Doreen Mshana ambao wanaendelea na
mazoezi ya viungo katika makazi yao mapya mjini Sioux IA baada ya
kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Mercy, Marekani.Sadia ambaye
hakuwahi hata kunyanyua mguu leo ameweza kufanya hivyo kwa mara ya
kwanza wakati akiendelea na mazoezi ya viungo.
Mbunge
wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye ana mchango mkubwa kwa
safari ya wanafunzi hao Marekani, amebainisha hilo katika ukurasa wake
wa Facebook.“Mtoto Sadia Atembea kwa kupanda ngazi kwa mara ya kwanza.
Praise
the Lord...aanza rasmi mazoezi ya kutembea,”ameandika Nyalandu.Jana
Nyalandu ambaye amekuwa akitoa taarifa za maendeleo ya wanafunzi hao
kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Facebook na Twitter,
jana aliandika kuwa pamoja na mazoezi ya viungo, watoto hao wanaanza
kufundishwa kwa saa moja kila siku saa 9 alasiri.
Alisema
wazazi wao walioambatana nao kwenye safari hiyo wanaanza darasa la
lugha kwa saa moja kila siku saa 3.00 asubuhi.“Tunawashukuru walimu wote
waliojitolea kwa kazi hii. Tuendelee kuwaombea watoto wetu,”aliandika
Nyalandu.
Comments