BAJETI MPYA:kodi za Road license,gesti zaondolewa usafirishwaji wa madini moja kwa moja wasitishwa


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
 
Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.Pamoja na hayo, Waziri Mpango ameshuha ushuru kwa mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu zinazozalishwa ndani kutoka Sh202 kwa lita hadi Sh200 kwa lita.
 
Kadhalika ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Sh429 hadi 450 kwa lita.
Wakati huo, ushuru wa bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka Sh534 hadi Sh564 kwa lita.
 
Ushuru nyumba za wageni.....
 
Serikali imetangaza kufuta ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala wageni.Hayo yalielezwa hapo jana (Alhamisi) bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango wakati akiwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18.
 
Pamoja na ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali zinapopatikana huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.
 
Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.
 
Usafirishaji wa madini...
 

Serikali imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.Hayo yameelezwa leo Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.
 
Badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa nje.“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.
 
una maoni gani mdau kuhusu hili?

Comments

Popular posts from this blog

Diamond atangaza kufunga ndoa mwaka huu