Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya
Armata ni kifaru cha kisasa ambacho kinachukua nafasi ya vifaru vya enzi za muungano wa Usovieti
Urusi
imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya
mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita.Vifaru hiyo vipya vya
Urusi kwa jina Armata T-14 vinaundwa vikiwa na teknolojia ya Kinga
Dhidi ya Makombora (APS).Lengo la teknolojia hiyo ni kuwezesha vifaru
hivyo kutoharibiwa na makombora mengi yaliyoundwa kukabiliana na vifaru,
yakiwemo yale aina ya Javelin yanayoundwa Marekani, ambayo yanatumiwa
na jeshi la Norway.
Brigidia Ben Barry wa taasisi kuhusu usalama wa kimataifa ya International Institute for Strategic Studies (IISS) mjini London anasema mataifa yanafaa kuanza kufikiria upya mifumo ya kukabiliana na makombora.
Anasema
mataifa mengi ya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi (Nato)
hayajagundua tatizo linalowakabili.Teknolojia ya APS inatishia kufanya
silaha nyingi za kukabiliana na vifaru kutofanikiwa, na mataifa mengi ya
Magharibi hayajaanza kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu hatua za
kuchukua.
Anasema
baadhi ya nchi zinafanya utafiti na majaribio kivyake kuweka mfumo huo
wa APS kwenye vifaru vya mataifa hayo."Lakini yanakosa kuzingatia
matokeo ya teknolojia hii kwa mfumo wao wa kukabiliana na vifaru,"
anasema.Norway ni moja ya nchi za kwanza kukumbana na hatari hii.Nchi
hiyo inapanga kutumia krona 200-350 milioni (£18.5-32.5 milioni; $24-42
milioni) kubadilisha makombora yake ya Javelin na "kudumisha uwezo wake
wa kukabiliana na vifaru"."Kuna haja ya kuwa na makombora ambayo
yanaweza kupinga mfumo wa APS."
- Adui anarusha kombora au mzinga kushambulia kifaru
- Mfumo kwenye kifaru unagundua kuna tishio njiani
- Teknolojia ya rada inahesabu njia na pahali palipolengwa
- APS inarusha kombora la kuharibu kombora au mzinga
- Kombora au mzinga wa adui unaharibiwa
Teknolojia
ya APS imebadilisha mambo katika historia ya kuangazia kushambulia na
kujilinda wakati wa vita.Katika vipindi fulani, kuna moja ambayo imekuwa
mbele.Zamani, vifaru visivyoweza kupenya risasi vilitawala, lakini
makombora nayo yakaimarishwa na kumaliza ubabe huo.Tangu Vita Vikuu vya
Pili vya Dunia, vifaru vimeendelea kutawala katika uwanja wa vita.Vifaru
hata hivyo, huwa vinaweza kuharibiwa na makombora au mabomu ya vifaru
vingine vikiwa karibu.
Lakini
kulikuwa pia na tishio kutoka kwa silaha nyingine, mfano makombora ya
kurushwa kutoka mbali au kutoka kwa ndege, jambo ambalo ndilo teknolojia
ya APS imeundwa kukabili.
Vifaru vya Israel aina ya Merkava huwa na teknolojia ya APS
Israel
ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa yakiongoza katika teknolojia ya
kujikinga na vifaru vyake aina ya Merkava hutumia teknolojia hii.Vifaru
hivyo vilitumiwa kukabiliana na wapiganaji wa Kipalestina ukanda wa
Gaza.Mfumo huo wa Israel pia unachunguzwa na Wamarekani.Uingereza pia
imeanza kutafakari uwezekano wa kustawisha teknolojia kama hiyo.Uholanzi
imeamua kutumia teknolojia nyingine, pia kutoka Israel, kukinga vifaru
vyake.
Comments